Red Devils na Liverpool kuumiza nyasi wikendi hii


Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 

2021/22 English Premier League

Matchday 9 of 38

Manchester United vs Liverpool 

Old Trafford 
Manchester, England
Sunday, 24 October 2021
Kick-off is at 18:30 

Manchester United watafufua uhasama wao na Liverpool Jumapili hii kwa mara ya kwanza msimu huu wa 2021/22 ugani Old Traffod.

Ole Gunnar Solskjaer
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Baada ya kuchapwa na Leicester City kwenye mchezo uliopita wa ligi, The Red Devils hawajashinda mechi yoyote kati ya tatu zilizopita. Matokeo duni ya Manchester United yanazidi kumuweka shinikizo meneja Ole Gunner Solskjaer na atakuwa na matumaini timu yake kupata ushindi dhidi ya timu ya Liverpool ambayo kwa sasa inaonekana mlima mkubwa kukwea.
 
“Ukiangalia mechi yenyewe vizuri, magoli manne toliyoruhusu hayakustahili,” Solskjaer alikiambia kituo cha habari cha Sky sports. “Tulivyocheza mechi hii hatustahili kuendelea bila kushindwa ugenini.


“Hivi karibuni tumekuwa na msururu usiokuwa mzuri. Hili ni jambo tunalotakiwa kulitazama kwa umakini kwa sababu tumepoteza alama nyingi kupita kiasi. Pengine tutahitaji mabadiliko na kuongeza bidii zaidi, au ni kitu gani tunatakiwa kufanya tofauti?


“Siwatetei wachezaji waliocheza, ni wachezaji wazoefu na hatujapata matokeo mazuri,” aliongeza. “Ujumla mchezo wete haukuwa mzuri. Magoli mawili kutokana na mikwajo ya adhabu inatamausha sana.”
 
Kwa upande wa pili, Liverpool ndiyo timu ya pekee kutopoteza mechi yoyote ya ligi msimu huu na wamewaacha United na alama nne baada ya kuwacharaza Watford mabao matano kwa sifuri. Roberto Firmino alifunga magoli matatu katika mechi hiyo ambayo Mohamed Salah aliendelea kujitangaza kama mchezaji bora ulimwenguni kwa sasa ukizingatia uchezaji binafsi.


“Nani bora kuliko yeye (Salah)? bila kuzungumzia utawala katika soka wa Messi na Ronaldo, sasa hivi Salah ndiye bora,” Jurgen Klopp alisema na shirika la habari la BT akiwa na furaha.


“Uchezaji wake leo ulikuwa mzuri sana. Pasi aliyotoa kwa mfungaji wa kwanza na goli alilofunga lilikuwa spesheli. Kwa sasa ndiye bora na sote tunalishuhudia.
 
Akizungumzia uchezaji wa timu kwa ujumla, Klopp alisema, “Baada ya mapumziko ni vigumu kupata uhuiano baada ya kucheza kwa mifumo tofauti lakini wachezaji wangu walishirikiana vizuri licha ya kuwa na muda mchache wa mazoezi kabla ya leo.”

Roberto Firmino
Hakimiliki ya picha: Getty Images 
 

Msimu uliopita, Liverpool walitoka sare nyumbani na kushinda united ugenini Old Trafford na kupata jumla ya pointi nne kutoka kwa Manchester United.
 

Takwimu baina ya Manchester United vs Liverpool

 
Mechi: 181
Manchester United: 70
Liverpool: 60
Sare: 51
 

Ratiba ya English Premier League, mechi ya 9

 
Oktoba 22 Ijumaa 
 
22:00 - Arsenal vs Aston Villa
 
Oktoba 23 Jumamosi
 
14:30 - Chelsea vs Norwich City 
17:00 - Crystal Palace vs Newcastle United 
17:00 - Leeds United vs Wolverhampton Wanderers 
17:00 - Everton vs Watford 
17:00 - Southampton vs Burnley 
19:30 - Brighton & Hove Albion vs Manchester City 
 
Oktoba 24 Jumapili
 
16:00 - West Ham United vs Tottenham Hotspur 
16:00 - Brentford vs Leicester City 
18:30 - Manchester United vs Liverpool


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 10/21/2021