76ers kuwakabili Timberwolves


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Philadelphia 76ers v Minnesota Timberwolves

2021-22 NBA Regular Season

Sunday 28 November 2021

Wells Fargo Center, Philadelphia, Pennsylvania

Tip-off at 02:00  

 

The Philadelphia 76ers watakabiliana na Minnesota Timberwolves katika mechi ya msimu ya NBA kwenye uwanja wa Wells Fargo Center uliopo Philadelphia. Mechi hiyo itang’oa nanga majira ya saa saba asubui ya jumapili Novemba 28 2021 saa za afrika ya kati.

 

Wikendi iliyopita, The 76ers walishinda Denver Nuggets kwa vikapu 103-89 na kuvunja msururu wa mechi tano bila ushindi. Ushindi huu ulikuja licha ya kumkosa Joel Embiid na wachezaji wengine watatu na sasa wanakaribia kilele cha jedwali la Eastern Conference.


Anthony Edwards
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Mchezaji Charles Bassey alisaidia sana kumdhibiti Nikola Jokic na vile vile kusaidia katika kupatikana kwa alama 12. “Baada ya kukosa huduma za Joel Embiid, nilijua fika wakati wa kuonyesha uwezo wangu umefika,” alisema Bassey. “Nilikuwa nimejiandaa.”

 

Timberwolves wamekuwa na matokeo mseto Western Conference, ingawaje walipata ushindi wa 115-90 dhidi ya San Antonio Spurs wikendi iliyopita wakiwa nyumbani ambapo Karl-Anthony Towns alionyesha mchezo mzuri na kuipa timu hiyo alama 25. Kocha Chris Finch wa Minnesota alifurahishwa na safu ya ulinzi wa timu hiyo.


Joel Embiid
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

"Walifanikisha mambo yote tuliyokusudia. Walijiandaa vizuri na kujituma na safu yetu ya ulinzi ilikuwa imara kabisa kwa maoni yangu,” alisema Finch ambaye alisifia timu nzima kwa kuimarika. “Mchezo wetu ulikuwa dhabiti katika kila sekta, kuanzia kushambulia, mtiririko na pia katika safu ya ulinzi. Imechukua muda kufikia kiwango hiki lakini sasa wakati umefika kwetu kuonyesha hiki kiwango mara kwa mara.”

 

Historia inaonyesha kwamba 76ers na Timberwolves wamekutana mara sitini katika mechi za msimu kuanzia mwaka 1989-90. Philadelphia wameshinda mara 31 huku 29 ikiwa kwa faida ya Minnesota. Timu hizi zilikutana mara ya mwisho katika mechi ya msimu Aprili 2021 ambapo 76ers waliibuka na ushindi. Ushindi huu ulikuwa ni wa nane mfululizo dhidi ya mahasimu hao. Tobias Harris aliipatia timu hiyo alama 32 katika ushindi huo wa 122-113, nyumbani.

 

Philadelphia 76ers v Minnesota Timberwolves – Head-to-head, Regular Season

Mechi: 60

76ers: 31

Timberwolves: 29

 

Bashiri Mpira wa Kikapu na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni mpira wa miguu, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.




Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.



 

Published: 11/26/2021