Hakimiliki ya picha: Soka La Bongo
Achana na Simba kukosa ubingwa kwa mara ya tatu mfululizo kuanzia
msimu wa 2021/22, 2022/23 na msimu huu, lakini wana Msimbazi wamepitia nyakati ngumu zaidi kuanzia pointi hadi mabao ya kufunga mbele ya mabingwa, Yanga huku namba na ufanisi uwanjani pia vikiwa mtihani kwa Simba.
Yanga imetwaa taji la 30 na la tatu mfululizo msimu huu ikiandika rekodi nyingi kuanzia kufunga mabao mengi, kukusanya pointi nyingi na kuzifunga timu zote 15 inazocheza nazo mashindano hayo, lakini kwa upande wa Simba mambo ni magumu.
Mbali na Yanga kuipita Simba kwenye kutwaa taji msimu huu, pia imewapita wapinzani wao kwenye maeneo haya.
KUONGOZA LIGI
Yanga imetwaa taji ikimtesa Simba kwenye nafasi ya kuongoza msimamo, Simba msimu huu imekaa kileleni mwa msimamo mzunguko wa tano tangu hapo vita ikawa kati ya mabingwa na Azam FC.
Misimu miwili nyuma ambayo Yanga ilitwaa ubingwa Simba ndio timu ambayo ilikuwa inakamata nafasi ya pili tofauti na msimu huu ambao inalega lega na kuingia vitani na Azam FC kuwania nafasi hiyo.
POINTI 10 NYUMA YA YANGA
Yanga imetetea taji la msimu huu ikiwa bado ina michezo mitatu mkononi hii ni baada ya kuwafunika wapinzani wake Simba na Yanga kwenye ukusanyaji wa pointi kwenye mechio walizocheza.
Yanga msimu huu imechukua pointi kwa timu zote 15 hivyo imefanikiwa kukusanya pointi nyingi kwenye mechi 26 wamekusanya pointi 68 huku watani wao Simba wao kwenye michezo 26 wana pointi 57 wakiachwa nyuma kwa pointi 10.
KURUHUSU MABAO
Wakati Yanga ikitangazwa kuwa mabingwa wa msimu huu tayari ilikuwa imeruhusu mabao 13 huku Simba nyavu zao zikitikiswa mara 24 kati ya mechi 26 walizocheza.
Ukuta wa Simba unaundwa na mabeki wa kati wa kigeni Henock Inonga na Che Malone Fondoh, huku upande wa Yanga imeruhusu idadi ndogo ya mabao ukuta wao ukiundwa na wazawa Ibrahim Hamad 'Bacca', Bakari Mwamnyeto wakisaidiana na Dickson Job.
KUTOA POINTI SITA KWA WATANI
Baada ya miaka mingi kupita msimu huu Yanga ikiwa bora imefanikiwa kukusanya pointi sita kutoka kwa watani wao Simba baada ya kuwafunga nje ndani.
Simba mbali na kutoa pointi zote sita dhidi ya Yanga imeweka rekodi ya kufungwa mabao saba ndani ya msimu mmoja wakikubali kichapo cha mabao
5-1 nyumbani na mzunguko wa pili walifungwa mabao 2-1.
SAFU YA USHAMBULIAJI
Msimu huu mabingwa ndio vinara wa upachikaji wa mabao wakiongozwa na kiungo wao mshambuliaji Stephane Aziz Ki ambaye amehusika kwenye mabao
23 kati ya 60 yaliyofungwa na timu yake akiingia kambani mara 15 na kutoa pasi za mwisho nane.
Yanga ambayo viungo ndio wanaongoza kupachika mabao imefunga mabao 60 kwenye michezo 26 waliyocheza huku watani zao Simba wao wakifunga mabao
51 wameachwa nyuma mabao tisa.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.