Verstappen apania kutetea taji la Monaco Grand Prix


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship 

Seven Round

2022 Monaco Grand Prix

Circuit de Monaco, Monaco
Monte Carlo and La Condamine, Monaco
Sunday, 29 May 2022
 
Max Verstappen anapania kutetea taji la mbio za langa langa za Monaco Grand Prix kwa mafanikio mnamo Mei 29.
 
Msimu uliopita, dereva huyo wa Red Bull Racing-RBPT alionyesha weledi wake kwenye mbio hizo na kushinda bila upinzani mkubwa.
 
Dalili zinaonyesha kuwa Verstappen atatetea taji la dunia la Formula One kwa mafanikio baada ya kupata ushindi wake wa tatu mfululizo, aliposhinda mbio za Spanish Grand Prix mnamo Mei 22.

Charles LeclercHakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Verstappen ambaye ni mzaliwa wa Hasselt, na mwana wa dereva wa zamani wa Formula One Jos Verstappen, alitumia fursa vizuri na kushinda mbio za Uhispania baada ya injini ya gari la Charles Leclerc wa Ferrari kupata hitilafu
 
Dereva mwenza Sergio Perez na George Russell wa Mercedes walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia katika mbio hizo za mzunguko wa sita wa msimu huu.
 
Kwa sasaVerstappen, anashikilia nafasi ya kwanza katika jedwali la 2022 la waendeshaji kwa mara ya kwanza na anatarajia kusalia kileleni hadi mwisho wa msimu.  
 
Leclerc na Perez wanashikilia nafasi ya pili na tatu mtawalia huku pambano la taji la dunia likipamba moto kuelekea mbio za Monaco Grand Prix.  

George Russell
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Akitathmini mbio za Spanish Grand Prix, Verstappen alikiri kufurahia mchuano wake na Russel kabla ya kuibuka na ushindi wa mbio hizo.
 
“Kwa kweli nilisumbuka kidogo kumpita Russel kutokana na hitilafu za DRS hata hivyo mchuano baina yangu na Russel niliufurahia,” Verstappen alisema.
 
"Nilifurahia zaidi nilipokuwa upande wa nje George akiwa upande wa nje na kisha nikarudi upande wa nje tena kwenye mzunguko wa tatu.
 
“Napata furaha nikitazama hali hiyo sasa; wakati huo nilisumbuka kidogo lakini ulikuwa mchuano mzuri na mgumu.”
 
Red Bull Racing-RBPT wanaongoza katika jedwali la waundaji wakifuatiwa na Ferrari huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Mercedes.
 

Matokeo ya mbio za langa langa za Monaco Grand Prix 2021

 
Mshindi: Max Verstappen of Red Bull Racing-Honda
Nafasi ya pili: Carlos Sainz Jr - Ferrari
Nafasi ya tatu: Lando Norris - McLaren-Mercedes 
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 05/26/2022