Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021/22 Spanish La Liga
Matchday 38
FC Barcelona v Villarreal CF
Camp Nou
Barcelona, Spain
Sunday, 22 May 2022
Kick-off is at 18h30 CAT
FC Barcelona watakuwa mwenyeji wa Villarreal CF ugani Camp Nou kwenye
mechi ligi mnamo Mei 22.
Barca waliambulia sare ya 0-0 ugenini dhidi ya Getafe CF kwenye mechi ya ligi iliyochezwa Mei 15.
Barcelona hawajashindwa katika mechi nne za ligi zilizopita huku wakiandikisha ushindi mara tatu mfululizo na sare moja.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Barca hawajapoteza mechi yoyote ya ligi kati ya mechi mbili za mwisho walizocheza wakiwa baada ya kuandikisha ushindi kwenye mechi zote mbili; dhidi ya Celta Vigo na Real Mallorca ugani Camp Nou.
“Leo tunachua nafasi ya pili rasmi katika msimamo wa ligi. Kwangu mimi tumetimiza malengo ya msimu huu kwa kufuzu kucheza ligi ya mabingwa msimu ujao na pia Spanish Super Cup,” alisema meneja wa Barcelona Xavi Hernandez baada ya sare na Getafe.
“Real Madrid walipata ubingwa wa ligi na hatukuweza kupambana nao. Hatukupambana vilivyo kwenye mashindano mengine. Kwa kupata nafasi ya pili katika ligi ni mafanikio makubwa ukizingatia msimu wetu ulivyoanza.
“Mechi ya leo ilikuwa ngumu. Sare hii imesaidia timu zote mbili. Awali tulipata habari kuwa Sevilla na Atletico walitoka sare.”
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwingineko, Villarreal walipoteza mechi yao ya ligi 2-1 wakiwa nyumbani dhidi ya Real Sociedad. Mechi hiyo ilichezwa Mei 15.
Kabla ya mechi hiyo, Villarreal walikuwa hawajashindwa kwenye mechi mbili za mwisho za ligi huku wakipata sare moja na ushindi mmoja.
Villarreal wamekuwa na matokeo mseto katika mechi za ligi ugenini. Wameandikisha ushindi mara mbili na kushindwa kwenye mechi moja katika mechi tatu zilizopita.
Barcelona na Villarreal walikutana mara ya mwisho katika ligi mnamo Novemba 27 2021.
Barcelona walipata ushindi wa 3-1 dhidi ya Villarreal kwenye mechi hiyo iliyochezewa ugani Estadio de la Cerámica ambao ulifahamika kama El Madrigal zamani.
Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi
Mechi - 5
Barcelona - 5
Villarreal - 0
Sare - 0
Ratiba ya La Liga mchezo wa 38
Mechi zote kuanza 7:30pm
Mei 22 Jumapili
Real Madrid v Real Betis
CA Osasuna v Real Mallorca
Sevilla FC v Athletic Bilbao
Granada CF v RCD Espanyol
Valencia CF v Celta Vigo
Real Sociedad v Atletico Madrid
Rayo Vallecano v UD Levante
Elche CF v Getafe CF
Deportivo Alaves v Cadiz CF
FC Barcelona v Villarreal CF
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.