Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 The Players Championship
US PGA Tour
TPC Sawgrass
Ponte Vedra Beach, Florida, USA
11-13 March 2022
Justin Thomas yupo tayari kutetea taji la
Players Championship kule Ponte Vedra Beach, Florida, nchini Marekani.
Mmarekani huyo alishinda taji hilo mwaka jana baada ya kumshinda Lee Westwood.
Thomas ambaye kwa sasa anashikilia nafasi ya nane katika jedwali la dunia la golfu, atakuwa mchezaji wa kwanza kutetea taji la Players Championship kwa mafanikio iwapo atashinda shindano la mwaka huu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Kwa wastani, mchezaji huyu hushinda angalau taji moja la shindano la PGA Tour tangu mwaka 2017 baada ya kushinda mashindano matano katika msimu wa 2017 – 2018 wa PGA Tour.
Thomas alishinda shindano la CJ Cup la mwaka 2019 nchini Korea ya Kusini na kuwa mchezaji wa mwaka kwa mara ya pili tangu shindano hilo kuasisiwa miaka mitatu iliyopita.
Mchezaji huyo mwenye makao yake kule Florida, alishinda shindano la WGC-FedEx St. Jude Invitational 2020 lililoandaliwa TPC Southwind Tennessee baada ya kuwapiku wachezaji wengine wannne.
Shindano la mwisho la PGA Tour kushindwa na Thomas lilikuwa Players Championship mwaka jana na sasa anatarajia kushinda taji lake la kwanza la mwaka 2022 kwenye TPC Sawgrass.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
“Ni vitu vingi vidogo,” alisema Thomas, ambaye ni mshindi mara mbili wa PGA Tour, kuhusu kuimarika kwake kuelekea mwaka 2022.
“Kwa bahati mbaya au nzuri, ushindi ndio unatumika kupima uwezo wa mchezaji. Kwa maoni yangu, nafaa kushinda na kucheza kwa weledi katika mashindano makubwa.
“Naamini katika uwezo wangu na kuelewa kwamba ni kiwango changu kushiriki mashindano makubwa mara kwa mara. Sijakamilisha hayo kwa sasa.”
Jack Nicklaus ni mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika mashindano ya The Players Championship baada ya kushinda mara tatu shindano hilo.
Wachezaji watano wa mwisho wa Players Championship
2016 - Jason Day - Australia
2017 - Kim Si-woo - Korea Kusini
2018 - Webb Simpson - Marekani
2019 - Rory McIlroy - Northern Ireland
2021 - Justin Thomas - Marekani
Bashiri Gofu na Betway
Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.