Shindano la golfu la Valspar 2022 kung’oa nanga


Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

2022 Valspar Championship 

US PGA Tour 

Copperhead Course 
Innisbrook Resort and Golf Club 
Palm Harbor, northwest of Tampa, Florida, USA 
17-20 March 2022 
 
Shindano la Valspar 2022 linatarajiwa kuchezwa kati ya tarehe 17 na 20 Machi kwenye mkondo wa golfu wa Copperhead Course, Innisbrook Resort and Golf katika jimbo la Florida nchini Marekani.
 
Shindano hili liliasisiwa mwaka 2000 kwa jina la Tampa Bay Classic na sasa linadhaminiwa na Valspar Corporation ambayo ni kampuni ya Marekani ya kuzalisha rangi na bidhaa zake.
 
Ni moja kati ya shindano la PGA linalokuwa kwa kasi sana tangu lilipoanza kudhaminiwa na Valspar mwaka 2014. Shindano la 2020 lilifutiliwa mbali kutokana na janga la Covid-19.

Dustin-Johnson-in-action.jpg
Hakimiliki ya picha: Getty Images 

 
Sam Burns ndiye bingwa mtetezi wa shindano la golfu la Valspar baada ya kushinda mashindano yam waka jana.  
 
Shindano la mwaka huu litajumuisha Burns, Paul Casey, Scottie Scheffler, Justin Thomas, Collin Morikawa, Dustin Johnson na wengineo.
 
Shindano litakuwa na wachezaji 144 na litachezwa kwa muda wa siku nne likiwa ni shindano la 21 katika ratiba ya PGA Tour msimu wa 2021-2022.
 
Washindi wa zamani wa shindano hili la Valspar Adam Hadwin, Charl Schwartzel, Kevin Streelman na Luke Donald watakuwa miongoni mwa washiriki.
 
“Huu ndio mwanzo tu wa maandalizi ya shindano ambalo tunaami litakuwa la kusisimua,” alisema mkurugenzi wa shindano la Valspar Tracy West.
 
“Wapenzi na mashabiki wa Copperhead wakiwepo mabingwa wa zamani wajiandae kushuhudia shindano wiki zijazo. 
 
"Ni matumaini yetu kuwa tutakuwa na mashabiki wapya kushuhudia shindano hili.”
 
Casey, K.J Choi na Retief Goosen ndio wachezaji wenye mafanikio makubwa katika historia ya mashindano ya golfu ya Valspar huku wakiwa wameshinda mara mbili kila mmoja.
 

Washindi 5 wa mwisho wa Valspar Championship

 
2016 - Charl Schwartzel - Afrika Kusini
2017 - Adam Hadwin - Canada
2018 - Paul Casey - England 
2019 - Paul Casey - England
2021 - Sam Burns - Marekani 
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 
 

Published: 03/18/2022