Man United na mpango wa kuwaondoa Atletico


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2021/22 UEFA Champions League 

Round of 16 - Second-Leg 

Manchester United v Atletico Madrid 

Old Trafford 
Manchester, England 
Tuesday, 15 March 2022
Kick-Off 21h00  
 
Manchester United watakuwa mwenyeji wa Atletico Madrid katika mechi ya  UEFA raundi ya 16 mkondo wa pili Machi 15.
 
Mchezo wa kwanza baina ya timu hizo mbili ulitoka sare ya 1-1 ugani Estadio Wanda Metropolitano, Uhispania huku Atletico wakiwa nyumbani Februari 23.
 
United hawajashindwa mechi yoyote katika sita za mashindano haya baada ya kuandikisha ushindi katika mechi tatu na kupata sare tatu.

Ralf Rangnick
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Wakiwa nyumbani, United wameandikisha ushindi mara mbili mfululizo na kupata sare moja katika mechi tatu za UEFA za mwisho.
 
"Kipindi cha kwanza hatukuwa na mchezo mzuri lakini baada ya kufanya mabadiliko mchezo wetu uliimarika kipindi cha pili,” alisema winga wa United Anthony Elanga baada ya kufunga dhidi ya Atletico.
 
"Ralf Rangnick aliniambia nitumie nafasi zozote nitakazopata na kuwapa wakati mgumu walinzi wa Atletico. Nimeshaonyesha utulivu wangu. Nataka kuonyesha uwezo wangu asilimia 150 kila nikipata nafasi ya kucheza. Huwa najiambia kuwa nataka kuwa mchezaji bora uwanjanai.”
 
"Nafikiri ilikuwa ni mara yangu ya kwanza kugusa mpira. Ilikuwa ni ndoto yangu kufunga katika mechi ya UEFA dhidi ya timu kubwa kama Atletico Madrid. Kila nikipata nafasi ya kuwa uwanjanai nitalipa heshima ya kocha kunipa nafasi hiyo,” aliongezea.
 
"Nilitarajia tutawapa mashabiki wetu matokeo mazuri, hasa waliosafiri mwendo mrefu. Natumai mkondo wa pili Old Trafford tutawapa matokeo mazuri zaidi.

Joao Felix
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Kwengineko, Atletico watakuwa na mpango wakuwashinda United nyumbani Old Trafford ili kufuzu hatua ya robo fainali.
 
Mabingwa hao wa Uhispania hawajashindwa katika mechi mbili zilizopita kwenye shindano hili baada ya kuandikisha ushindi mmoja na sare moja.
 
Hata hivyo, Atletico wamekuwa na matokeo mseto ugenini katika shindano hili huku wakiandikisha ushindi mara tatu na kushindwa mechi mbili katika michezo mitano iliyopita.
 
Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa United kuwaalika Atletico.
 

Takwimu baina ya timu hizi mbili

 
Mechi - 1
United - 
Atletico - 0
Sare - 1


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 03/14/2022