Moto GP - 2023 Dutch TT Assen


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 MotoGP Season

2023 Dutch TT Assen

Round 8
TT Circuit Assen
Assen, Netherlands 
Sunday, 25 June 2023
 
Francesco Bagnaia anatarajia kuwa mwendesha pikipiki wa kwanza kushinda mbio za Dutch TT Assen mara mbili mfululizo tangu Valentino Rossi kufanya hivyo mwaka 2005 na 2004. 
 
Mbio za hivi karibuni
 
Mwendeshaji huyo wa Ducati wa timu ya Lenovo alichukua nafasi ya pili katika mbio za kusisimua za German MotoGP Juni 18.
 
Bagnaia mwenye jina la utani la Pecco, alianza katika kikundi cha kwanza lakini akapoteza nafasi hiyo ya kwanza kwa mwendeshaji mwenza wa Ducati mwishoni mwa mbio.
 
Mbio za 2022 za Dutch TT Assen 
 
Pecco alikuwa na mbio za kufana za Dutch TT Assen mwaka jana kwani alianza katika nafasi ya kwanza na kumaliza katika nafasi hiyo bila ushindani mkubwa.
 
Ni mbio alizopata mafanikio makubwa raia huyo wa Italia baada ya kumaliza katika nafasi ya 6 mwaka 2021, kukosa kushiriki mbio hizo mwaka 2020 na kumaliza katika nafasi ya 14 aliposhiriki mbio za pikipiki kwa mara ya kwanza mwaka 2019.  
 
Ishara zinaonyesha Bagnaia anaweza kushinda mbio za 2023 za Dutch TT Assen 
 
Bagnaia anapigiwa upatu kushinda mbio hizo kwani anashikilia nafasi ya kwanza kwenye jedwali la waendeshaji na anafanya kila juhudi kutetea taji la dunia la mbio za pikipiki, MotoGP.
 
Pecco ambaye ameshinda mbio tatu za msimu huu wa MotoGP atakuwa na kila sababu ya kuamini ataibuka na ushindi wa mbio hizo za mkondo wa TT baada ya kushinda mbio za mwaka jana.
 
Nukuu
 
"Nilifurahia mbio hizo sana. Zilifurahisha sana kuliko jana na zilikuwa na ushindani mkubwa. Nilijaribu kila mbinu lakini Jorge akanizidi maarifa,” Bagnaia alisema baada ya mbio za  German MotoGP.
 
"Niliongeza juhudi katika mizunguko ya mwisho lakini sikupata nafasi ya kumpita. Nilijiweka katika nafasi nzuri ikisalia mizunguko miwili ila nilimgusa kidogo na kupoteza mwelekeo kidogo. Nimefurahi mbio zilivyoenda kwa ujumla.
 
"Hatua tulizopiga jana ni kubwa na tunastahili kuwa na furaha. Nilijaribu kuwa katika nafasi ya kwanza ila juhudi zake hazikunipa nafasi. Bado tunayo nafasi ya kupigania taji iwapo tutafanya kila jambo ipasavyo na kuzingatia upande wetu.”
 

Matokeo ya 2022 ya Dutch TT Assen.

Mshindi: Francesco Bagnaia - Ducati
Nafasi ya pili: Marco Bezzecchi - Ducati
Nafasi ya tatu: Maverick Vinales - Aprilia
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 06/23/2023