Verstappen atarajia ushindi wa sita Montreal


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 FIA Formula One World Championship

2022 Canadian Grand Prix

Circuit Gilles Villeneuve
Notre Dame Island, Montreal, Canada
Sunday, 19 June 2022
 
Dereva wa Red Bull Racing Max Verstappen anatarajia kuendeleza msururu wa matokeo mazuri msimu huu wa Formula One atakaposhiriki mbio za Canadian Grand Prix Jumapili June 9. 
 
Verstappen ambaye ni bingwa mtetezi wa dunia anaongoza jedwali la madereva baada ya kushinda mbio tano kati ya mbio nane za kwanza na kumaliza mara sita jukwaani. 
 
Verstappen alifanikiwa kumaliza mbio moja tu kati ya tatu za kwanza za 2022. Hii ni baada ya kukatiza mbio za Bahrain Grand Prix na Australian Grand Prix kutokana na hitilafu za mkondo wa mafuta. 

Sergio Perez
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Verstappen ambaye ni raia wa Uholanzi alipata ushindi wa kwanza wa mwaka kwenye mbio za Saudi Arabian Grand Prix na kumaliza katika nafasi za jukwaani mara tano mfululizo mbio zilizofuata.
 
Verstappen akiwa na alama 150 anaongoza dereva mwenzake wa Red Bull Racing Sergio Perez kwa alama 21 baada ya kuchukua uongozi kwenye mbio za Emilia Romagna Grand Prix, Miami Grand Prix, Spanish Grand Prix na Azerbaijan Grand Prix na kumaliza katika nafasi ya tatu kwenye mbio za Monaco Grand Prix ambazo zilishindwa na Perez.
 
Dereva huyo mwenye umri wa miaka 24 amekiri alikuwa na bahati katika mbio za Baku baada ya madereva wa Ferrari Charles Leclerc na Carlos Sainz kupata hitilafu mapema kwenye mbio hizo na kujiondoa. 

Charles Leclerc of Ferrari
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Nadhani leo gari letu lilikuwa na udhabiti mkubwa. Magurudumu yalikuwa imara,” aliambia kituo cha Sky F1. 
 
"Vile vile tulikuwa na bahati kutokana na kujiondoa kwa Ferrari lakini hata hivyo gari letu leo lilikuwa na kasi hivyo basi ilikuwa rahisi kuwafikia. 
 
"Kwa ujumla nimefurahishwa na hali ya gari leo.” 
 

Matokeo ya mbio za Azerbaijan Grand Prix 2022

 
Mshindi: Max Verstappen - Red Bull Racing
Nafasi ya pili: Sergio Perez - Red Bull Racing
Nafasi ya tatu: George Russell - Mercedes
 

Bashiri Motosport na Betway


Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni sokamotorsportmpira wa kikapurugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 06/17/2022