Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023 Wimbledon Championships
ATP Tour
All England Lawn Tennis and Croquet Club
London, England
3–16 July 2023
Mchezaji nambari 6 duniani katika mchezo wa tenisi Holger Rune atakabiliwa na ushindani mkubwa kutoka kwa mchezaji nambari 1 duniani Carlos Alcaraz watakapokutana kwenye mechi ya robo
fainali ya shindano la Wimbledon.
Tayari mchezaji huyo mchanga kutoka Denmark amepata mafanikio makubwa kwenye shindano hilo mjini London linalochezewa kwenye sakafu ya nyasi baada ya kumgaragaza Grigor Dimitrov 3-6, 7-6, 7-6, 6-3 kwenye raundi ya nne.
Rune alibanduliwa kwenye raundi ya kwanza aliposhiriki kwa mara ya kwanza shindano la tenisi la All England Lawn Tennis and Croquet Club mwaka jana ila mchezo wake umezidi kuimarika siku hadi siku miezi 12 iliyofuata.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 ameshiriki fainali tatu za mashindano ya shirikisho la tenisi duniani (ATP Tour) mwaka hu una kushinda shindano la tenisi la Munich Open mwezi Aprili kabla ya kufuzu kuingia hatua ya robo fainali ya French Open kwa mara ya pili.
Rune alihitaji seti tano kumshinda Alejandro Davidovich Fokina katika raundi ya tatu baada ya kuwashinda George Loffhagen 7-6, 6-3, 6-2 na Roberto Carballes Baena 6-3, 7-6, 6-4 katika raundi za kwanza mbili.
Alitoa heshima yake kwa Dimitrov kwa ushindani aliompa walipokutana Julai 10 ila lengo lake lilikuwa kufika fainali yake ya kwanza ya Grand Slam huku mpinzani anayefuata akiwa Alcaraz.
"Mechi ya leo haikuwa rahisi. Grigor ni mchezaji mzuri na amenipa ushindani mkali. Upinzani ulikuwa mkali kwa pande zote. Ulikuwa mchezo wa kusisimua na pia mchezo mgumu,” alisema Rune.
"Nitapambana hadi hatua ya mwisho. Hilo ndilo lengo langu hasa ninapokumbwa na changamoto. Shindano la Wimbledon huandaliwa mara moja kwa mwaka. Nitapambana ili kupata nafasi ya ushindi.”
Washindi watano wa mwisho wa Wimbledon.
2022 - Novak Djokovic (SRB)
2021 - Novak Djokovic (SRB)
2019 - Novak Djokovic (SRB)
2018 - Novak Djokovic (SRB)
2017 - Roger Federer (Uswizi)
Bashiri tenisi mtandaoni
Bashiri manguli kwenye michuano bora ya tenisi kutoka Wimbledon hadi Roland Garros. Jisajili leo na anza kubashiri kwenye machaguo tofauti ambayo tenisi inakupatia; kutoka 1x2 matokeo ya mechi, bashiri kwa mchezaji wako unayempenda hadi kwenye bashiri nyingi kama Mshindi wa Set. Chochote unachochagua kufanya, Betway ina chaguo kwaajili yako.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway