Hakimiliki ya picha: Getty Images
2023 Farmers Insurance Open
US PGA Tour
Torrey Pines Golf Course
San Diego, California, USA
25-28 January 2023
Scottie Scheffler anapigiwa upatu kushinda shindano la gofu la Farmers Insurance Open litakaloandaliwa Torrey Pines Golf Course.
Raia huyo wa Marekani anasalia katika nafasi ya pili kwenye jedwali rasmi la gofu duniani huku lengo lake likiwa kunyakua nafasi ya kwanza kutoka kwa Rory McIlory.
Scheffler hajafanikiwa ushindi msimu 2022-23 japo alikaribia ubingwa wa shindano la World Wide Technology Championship, Mayakoba ambapo alimaliza katika nafasi ya tatu.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mwaka 2022 ulikuwa wenye mafanikio kwa mchezaji Scheffler kwani alifanikiwa kushinda WM Phoenix Open, Arnold Palmer Invitational, WGC-Dell Technologies Match Play na shindano la Masters.
Septemba 2022 mchezaji huyo ambaye ni mzaliwa wa New Jersey alitajwa mchezaji bora wa mwaka wa PGA Tour 2022 na kutunukiwa tuzo la Jack Nicklaus kwa mara ya kwanza.
Vile vile, Scheffler aliweka rekodi ya msimu kwa kuingiza kipato cha dola 14,046,910 za kimarekani. Wachezaji 126 walipata zaidi ya dola milioni moja kwenye PGA Tour ya msimu 2021-22.
Mwanafunzi huyo wa zamani wa chuo kikuu cha Texas na ambaye ni mshindi mara nne wa PGA Tour anatazamia kuongeza idadi ya mataji hadi matano kwa kushinda taji la Farmers Insurance Open.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Scheffler alieleza kuwa alikuwa akifanyia kazi baadhi ya mambo kipindi cha mapumziko alipoulizwa wakati wa shindano la mwaka huu la Sentry Tournament of Champions mapema mwezi huu.
“Nafanyia mazoezi vitu vingi kuhusu mchezo huu na juhudi zinaonekana kuzaa matunda,” alisema Scheffler.
"Najaribu kujiweka vizuri na kujiandaa kwa ajili ya mwaka mpya. Nimeanza vizuri n ani tumaini langu nitaendelea vivyo hivyo michezo ijayo.”
Tiger Woods ndiye mchezaji mwenye mafanikio makubwa katika historia ya shindano hili la Farmers Insurance Open akiwa na mataji saba.
Washindi watano wa mwisho wa shindano la Farmers Insurance Open
2018 - Jason Day - Australia
2019 - Justin Rose - Uingereza
2020 - Marc Leishman - Australia
2021 - Patrick Reed - Marekani
2022 - Luke List - Marekani
Shinda na Kombe la Dunia
Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.