Napoli na nia ya kuizima Juventus


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022/23 Italian Serie A 

Matchday 18

SSC Napoli vs Juventus FC 

Stadio Diego Armando Maradona 
Naples, Italy 
Friday, 13 January 2023 
Kick-off is at 21h45 
 
SSC Napoli watakuwa mwenyeji wa Juventus FC katika mechi ya ligi kuu Italia ugani Stadio Diego Armando Maradona Januari 13.
 
Napoli, maarufu kama The Little Donkeys walinyakua ushindi wa 2-0 nyumbani dhidi ya UC Sampdoria katika mechi ya ligi ya Januari 8.
 
Ulikuwa ni ushindi wa pili wa Napoli katika mechi tatu za mwisho za ligi huku wakipoteza mchezo wa tatu dhidi ya Inter Milan kabla ya kukutana na Sampdoria.

Khvicha Kvaratskhelia
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
Napoli hawajapoteza mchezo wa ligi katika michezo 11 ya mwisho wakiwa nyumbani huku wakiandikisha sare mbili na kushinda mechi tisa ugani Stadio Diego Armando Maradona.
 
Kwa upande mwingine, Juventus waliibuka na ushindi wa 1-0 nyumbani dhidi ya Udinese Calcio katika mechi yao ya mwisho ya ligi Januari 7.
 
Ushindi huo ulikuwa wa nane mfululizo katika mechi nane za ligi za mwisho kwa timu hiyo ya Juventus.
 
Vile vile, Juventus hawajapoteza mchezo wa ligi katika michezo minne ya mwisho wakiwa ugenini baada ya kuandikisha ushindi mara nne mfululizo.

Massimiliano Allegri
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 
 
"Tuko katika kipindi kizuri ukizingatia matokeo yetu. Tunastahili kuimarika zaidi kwenye uchezaji wetu,” alisema meneja wa Juventus Massimiliano Allegri baada ya ushindi dhidi ya Udinese.
 
"Hatukuwa na umakini wa kiwango kinachostahili katika ushindi wetu wa 1-0 dhidi ya Cremonese Jumatano lakini tulimakinika vizuri dhidi ya Udinese ambaye ni mpinzani dhabiti. Tulitengeneza nafasi nyingi katika kipindi cha pili.
 
"Napoli wana nafasi kubwa ya kushinda ligi katika hali ilivyo ilhali tunapambania kumaliza nne bora. Tunafanya vizuri ikiwa ni takriban nusu ya msimu.”
 
Mechi ya mwisho ya ligi baina ya Napoli na Juventus ilikuwa Januari 6 2022.
 
Mchezo huo uliishia sare ya 1-1 na ulichezewa Allianz Stadium ambao ni uga wa nyumbani wa timu ya Juventus uliofunguliwa mwaka 2011.
 

Takwimu baina ya timu hizi, mechi tano za mwisho za ligi.

Mechi - 5
Napoli - 3
Juventus - 1
Sare - 1
 

Ratiba ya mechi za Serie A mchezo wa 18.


Januari 13 Ijumaa

10:45pm - SSC Napoli v Juventus FC

Januari 14 Jumamosi

5:00pm - US Cremonese v AC Monza
8:00pm - UC Lecce v AC Milan
10:45pm - Inter Milan v Hellas Verona

Januari 15 Jumapili

2:30pm - Sassuolo v SS Lazio
5:00pm - Torino FC v Spezia Calcio
5:00pm - Udinese Calcio v Bologna FC
8:00pm - Atalanta BC v US Salernitana
10:45pm - AS Roma v ACF Fiorentina

Januari 16 Jumatatu

10:45pm - Empoli FC v UC Sampdoria
 

Chomoka na Odds na ushinde zawadi kubwa​

Siku 60 za kwanza za Chomoka Odds zimekamilika, lakini msimu wa soka ndio kwanza umeanza, bado una nafasi ya kushinda pesa taslimu na Free Bet kila wiki, na bila shaka, zawadi kubwa ya Vifaa vya Nyumbani ikiwemo Tv, home theatre, jiko na mashine ya kufulia.Chomoka na Odds


Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama; Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.
 

Published: 01/11/2023