American Express 2022 kung’oa nangas


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 The American Express 

US PGA Tour 

PGA West Private Clubhouse & Golf Courses
La Quinta, California, USA 
20-23 January 2022
 
Mashindano ya mwaka huu ya American Express yatang’oa nanga kati ya tarehe 20 na 23 januari, PGA West Private Clubhouse & Golf Courses
 
Mashindano haya pia yanaitwa Dessert Classic na huu utakuwa ni mkondo wa 63 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1960.
 
Awali, shindano hili lilifahamika kama CareerBuilder challenge, Palm Springs Golf Classic, the Bob Hope Desert Classic, the Bob Hope Chrysler Classic na the Humana Challenge.  

Phil Mickelson
Hakimiliki ya picha: Getty Images

 
Kim Si-woo ndiye bingwa mtetezi wa shindano hili baada kushinda the American Express mwaka jana kwa kumpiku Patrick Cantlay.  
 
Shindano la mwaka huu litajumuisha wachezaji 156 waliochaguliwa kwa kuzingatia nafasi zao katika jedwali zinatambulika.
 
Cantlay na Jon Rahm walio katika nafasi ya kumi bora kwenye jedwali rasmi la golfu duniani watakuwa miongoni mwa washiriki kule PGA West Private Clubhouse & Golf Courses.
 
Mabingwa wa zamani wa American Express Phil Mickelson Bill Haas watashiriki pia huku wakinuia kushinda shindano hilo tena.
 
Ni furaha kubwa kwa waandaaji wa American Express 2022 kuwa na bingwa wa 2018 wa shindano hilo, bingwa wa sasa wa US Open na mshindi mara sita wa PGA Tour Rahm.
 
“Hakuna njia bora ya kutangaza zaidi mashindano haya kama kumshirikisha mchezaji wa golfu anayeshikilia nafasi ya juu ya mchezo huu hapa Coachella Valley,” alisema mtendaji mkuu wa American Express Pat McCabe.
 
“Ni furaha kubwa kumkaribisha Jon ambaye ni bingwa wa zamani wa shindano hili na atasaidia sana katika kuboresha shindano hili ambalo tayari ni kubwa.”
 
Arnold Palmer ndiye mwenye mafanikio makubwa zaidi katika historia ya mashindano haya baada ya kuyashindana mara tano.
 

Washindi watano wa mwisho wa American Express.

 
2015 - Hudson Swafford - Marekani
2018 - Jon Rahm – Uhispania
2019 - Adam Long - Marekani
2020 - Andrew Landry - Marekani 
2021 - Kim Si-woo – Korea kusini
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.


 

Published: 01/18/2022