KOCHA Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amesema ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kusonga mbele katika hatua ya makundi ya
Ligi ya Mabingwa Afrika ni lazima wapate ushindi wa mabao mengi dhidi ya wapinzani wao CR Belouizdad ya Algeria utakaochezwa Jumamosi ijayo, Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Gamondi amesema baada ya matokeo ya sululu kati ya CR Belouizad dhidi ya Al Alhly, Ijumaa iliyopita nchini Algeria, kundi limekuwa gumu kwao na kitu pekee kitakachofanya kujiweka kwenye nafasi nzuri ya kwenda robo fainali ni ushindi wa mabao mengi, kabla ya kubakisha mechi moja dhidi ya Al Ahly ugenini.
Katika kundi aliopo Yanga inashika nafasi ya tatu akiwa na alama tano sawa na CR Belouizdad ambaye yuko nafasi ya pili, Medeama FC akiwa nafasi ya nne kwa kukusanya pointi nne na Al Ahly anaongoxa kundi hilo akiwa na alama sita.
Yanga inahitaji ushindi wa idadi kubwa ya mabao dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria, watakaocheza Jumamosi hii uwanja wa Benjamin Mkapa Dar es Salaam ili kujiweka kwenye nafasi nzuri baada ya kukamilika kwa michezo ya kundi hilo.
Gamondi amesema wanafanya maandalizi mazuri kwa ajili ya kutafuta ushindi katika mchezo dhidi ya CR Belouizdad ili kujiweka katika nafasi nzuri katika msimamo wa kundi hili.
Amesema wako kwenye kundi ngumu ambalo kila timu ina nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali hali ambayo wanatakiwa kupambana na kuumiza kichwa ili kusaka ushindi mechi ya nyumbani.
"Hakika kila timu inaweza kwenda robo kulingana na kundi lilivyo, tunasahihisha makosa yetu, tumefanikiwa kufanya vizuri kwenye safu ya ulinzi lakini pia hata kushambulia kwa sababu ya kila mechi tumefanikiwa kufunga bao," amesema Gamondi.
Amesema mechi dhidi ya CR Belouizdad haitakuwa rahisi kwa sababu ya ugumu wa kundi hilo lakini pia baada ya kuwaona wapinzani wake katika mechi na Al Ahly.
"Nimefanikiwa kuangalia mechi yao na Al Ahly, nimeona ubora wao walicheza vizuri na tumeanzia mechi hiyo kufanya maandalizi yetu kuelekea mechi yetu ijayo.
Tumeona ubora wa wapinzani wetu na kulingana na kundi lilivyo tunahitaji kutafuta ushindi wa mechi ya hapa nyumbani ikiwezekana kufunga idadi kubwa ya mabao ili tujiweka katika nafasi nzuri ya kwenda robo fainali,”
amesema Kocha huyo.
Jisajili na Betway, burudika na kila tukio na amsha amsha ukibashiri kwenye ligi za mpira wa miguu kama;
Ligi Kuu ya Uingereza, La Liga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na mengi zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie
Betway kwenye kurasa zetu za
Facebook,
Twitter,
Instagram na
Youtube. Pakua App ya Betway.