Hakimiliki ya picha: Getty Images
2021 FIA Formula One World Championship
2021 Saudi Arabian Grand Prix
Jeddah Corniche Circuit
Jeddah, Saudi Arabia
Sunday, 5 December 2021
Max Verstappen wa Red Bull Racing-Honda atakuwa na nia moja tu, kushinda
mbio za langalanga Disemba 5 nchini Saudi Arabia.
Matumaini ya mdachi huyo kushinda mbio za Formula One msimu huu zilitiwa dosari alipomaliza katika nafasi ya pili mnamo Novemba 21 kwenye mbio za Qatar.
Hii ilikuwa ni mara ya pili kwa Verstappen kumaliza katika nafasi ya pili mfululizo, mara ya kwanza ikiwa ni mbio za Brazil Novemba 14.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Mbio za Qatar zilishindwa na Lewis Hamilton wa Mercedes, huku akiendelea kumenyana vikali na Verstappen kutafuta mshindi.
Verstappen anaendelea kuongoza katika jedwali la madereva huku akifuatiwa kwa ukaribu na mpinzani wake, Hamilton.
Dereva mwenza wa Mercedes, Valtteri Bottas anabakia katika nafasi ya tatu akifuatiwa na dereva mwenza wa Verstappen, Sergio Perez anayechukua nafasi ya nne katika jedwali la madereva.
Verstappen kwa sasa anamzidi Hamilton kwa alama nane tu na mshindi wa mbio za Saudi Arabia atakuwa kileleni huku ikisalia mbio moja msimu kukamilika.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
"Nilikuwa na hari ya kushindana nilipogundua nitaanza wa saba na hivyo ndivyo tulivyofanya,” alisema Verstappen baada ya mbio za Qatar.
"Mzuzunguko wetu wa kwanza ulikuwa mzuri na baada ya mzunguko wa tano tulikuwa katika nafasi ya pili tena. Nafasi kati yetu na kiongozi ilikuwa sio pana katika mbio hizo. Mwishowe kupata mzunguko wa kasi zaidi ilifurahisha. Nafahamu msimu ukielekea ukingoni hali itakuwa ngumu kidogo na ni vizuri kwa sababu mhemko utaongezeka.
"Mkondo huu una raha yake kuendeshea. Unaendana vizuri na magurudumu. Ushindani utakuwa wa karibu mpaka mwisho. Zimesalia mbio mbili na chochote kinaweza kutokea.”
Mercedes inaongoza kwa ujumla ikifuatiwa na Red Bull Racing-Honda huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na McLaren-Mercedes.
Matokeo ya mbio za langalanga za Qatar 2021.
Winner: Lewis Hamilton - Mercedes
Second-Place: Max Verstappen - Red Bull Racing-Honda
Third-Place: Fernando Alonso - Alpine-Renault
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.