US PGA - RBC Heritage


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2023 RBC Heritage  

US PGA Tour

Harbour Town Golf Links
Hilton Head Island, South Carolina, USA
13-16 April 2023
 
Shindano la gofu la RBC Heritage 2023 linatarajiwa kung’oa nanga kisiwani Hilton Head, jimbo la South Carolina kati ya tarehe 13 na 16 Aprili. 
 
Kuhusu shindano.
 
Shindano hili la PGA lilianzishwa mwaka 1969 likifahamika kama Heritage Golf Classic na limekuwa likichezewa Harbour Town Golf Links, South Carolina muda wote tangu lilipoasisiwa. 
 
Benki ya Royal ya Canada maarufu kama (RBC) imekuwa mfadhili wa shindano hili tangu mwaka 2012 na limekuwa likiandaliwa na wakfu wa The Heritage Classic Foundation.
 
Habari za shindano hili
 
Heritage Classic Foundation imetangaza kuwa bingwa mara tano wa RBC Heritage Davis Love III atakuwa mwenyekiti wa shindano la 2023 la RBC Heritage. 
 
Kwa kawaida, mwenyekiti wa shindano hili huwa mwanachama wa wakfu wa Heritage Classic. Ila kwa kusherekea shindano hili la 55, bodi ya wadhamini ilifanya maamuzi ya kujumuisha bingwa wa zamani wa shindano hili.  
 
Shindano hili litahusisha wachezaji 146 na litachezwa kwa siku nne huku wachezaji 43 waliopo hamsini bora kwenye jedwali rasmi la gofu duniani wakiwa miongoni mwa wanaopigiwa upatu kuibuka na ushindi.
 
Wanaopigiwa upatu kushinda.
 
Scottie Scheffler, Rory McIlroy na Jon Rahm ambao ni wachezaji watatu bora duniani muda huu katika mchezo wa gofu watashiriki shindano la mwaka huu la RBC Heritage.
 
Wataungana na bingwa mtetezi Jordan Spieth, mshindi wa 2020 Webb Simpson na bingwa mara tatu wa shindano hili Stewart Cink.
 
Mabalozi wa RBC Sam Burns, Corey Conners, Sahith Theegala na Cameron Young vile vile watakuwa miongoni mwa washiriki. 
 
Tuzo  
 
Mshindi wa shindano hili atazawadiwa alama tano zitakazoimarisha nafasi yake kwenye jedwali rasmi la gofu duniani. Viwango vya mwisho vitahakikiwa Alhamisi kabla ya shindano kuanza. 
 
Vile vile, kuna kiasi cha dola milioni 20 za kimarekani zitakazoshindaniwa huku mshindi akiondoka na dola milioni 3.6 na pia kombe la “Sir William Innes”.
 
Nukuu
 
Wakfu wa Heritage Classic umetangaza kuwa kampuni ya Coca-Cola Consolidated imeongeza mkataba wa miaka mitano kusambaza vinywaji visivyo na vileo kwenye shindano la RBC Heritage.
 
“Tunafurahi kufanya kazi na kampuni tajika ambayo ina historia ya kusaidia watu,” alisema rais wa Heritage Classic Foundation Steve Wilmot. 
 
"Ushirikiano wetu na kampuni ya Coca-Cola Consolidated kwa takribani miaka 25 umezidi kuwatuliza kiu watazamaji na wafadhili wetu.” 
 
Bidhaa za Coca-Cola zimekuwa zikitumika katika shindano hili la RBC Heritage tangu mwaka 1969.
 

Washindi watano wa mwisho wa RBC Heritage.

 
2018 - Satoshi Kodaira - Japan 
2019 - Pan Cheng-tsung - Taiwan 
2020 - Webb Simpson - Marekani 
2021 - Stewart Cink - Marekani 
2022 - Jordan Spieth - Marekani  
 

Shinda na Kombe la Dunia

Dunia imekusanyika kushuhudia michuano bora zaidi ya soka. Ingia kwenye Droo yetu ya Kila Siku ya Mechi ujishindie TSh 500,000 na ufurahie Free Predictor.

Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway. 

Published: 04/14/2023