Finau apania kushinda taji la Mexico Open


Hakimiliki ya picha: Getty Images

 

2022 Mexico Open

US PGA Tour 

Vidanta Vallarta
The Norman Signature Course 
Vallarta, Mexico 
28 April - 1 May 2022 
 
Tony Finau atapania kushinda taji la mashindano ya gofu ya 2022 ya Mexico Open ili kuimarisha nafasi yake kwenye jedwali rasmi la dunia la gofu. 
 
Kati ya washiriki wa shindano la mwaka huu, ni Jon Rahm na Abraham Ancer tu wanaomshinda Tony Finau katika jedwali. 
 
Raia huyo wa Marekani tayari ameshinda mashindano matatu tangu alipoanza kucheza gofu ya kulipwa akiwa na miaka 17 mwaka 2006. Mataji hayo yanajumuisha mashindano mawili ya PGA Tour.

Cameron Smith
Hakimiliki ya picha: Getty Images
 

Tony Finau anayeishi Arizona alishinda taji lake la kwanza la shindano la PGA Tour mwaka 2016, Puerto Rico Open alipomshinda Steve Marino kwenye muondoano dakika za mwisho kabisa. 
 
Finau, kisha alishinda shindano la Northern Trust Trophy la 2021 ikiwa ni Zaidi ya miaka mitano na mashindano 142 bila kushinda shindano lolote la PGA Tour. 
 
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 33 alijituma sana na kusaidiwa na ukosefu wa umakini kutoka kwa Cameron Smith kulimsaidia kupata ushindi kwenye mechi hiyo ya shindano la Northern Trust iliyocheleweshwa na mvua. 
 
Mwaka huu, Finau alimaliza katika nafasi ya 19 kwenye shindano la Sentry Tournament of Champions mwezi Januari ambayo yalikuwa matokeo duni ukilinganisha na alivyofanya katika shindano la mapema Aprili la Valero Texas Open.
 
Mchezaji huyo wa gofu amesema kuwa amejitahidi sana huku akitazamia kushinda mataji Zaidi ya PGA Tour.
 
“Ukakamavu ni jambo muhimu wakati huu ili kuvuka vikwazo na changamoto, sio kwenye gofu tu bali hata kwenye Maisha ya kawaida,” alisema Finau.
 
“Ni ukakamavu tu. Haijalishi nimefikia hatua gani. Kuna hizo hisia kwamba bado kuna nafasi ya kuimarika zaidi na kushinda changamoto. Ukakamavu pekee ndio umeniwezesha kufika nilipo.
 
"Ni mambo muhimu tunayopambana nayo katika mashindano ya PGA Tour.”
 
Al Espinosa ndiye mchezaji mwenye mafanikio zaidi katika historia ya Mexico Open akiwa ameshinda mashindano hayo mara nne.
 

Washindi watano wa mwisho wa Mexico Open

2016 - Justin Hueber - Marekani 
2017 - Sebastian Vazquez - Mexico 
2018 - Austin Smotherman - Marekani 
2019 - Drew Nesbitt - Canada 
2021 - Alvaro Ortiz - Mexico 
 

Bashiri Gofu na Betway

Ingia uwanjani mchomo mmoja ubashiri gofu na Betway. Betway inakuletea matukio yote ya gofu kutoka michuano mikubwa Duniani kote.



Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za FacebookTwitterInstagram na Youtube. Pakua App ya Betway.

Published: 04/26/2022