Hakimiliki ya picha: Getty Images
2022 MotoGP Season
2022 British Grand Prix
Round 12
Silverstone Circuit
Silverstone, England
Sunday, 7 August 2022
Mbio za pikipiki za
British Grand Prix 2022, zinazojulikana kama Monster Energy British Grand Prix pia zitang’oa nanga katika Kijiji kitwaacho Silverstone nchini Uingereza Agosti 7.
Hizi zitakuwa mbio za 12 za mashindano ya mwaka huu na zitafanyika kwenye mkondo wa Silverstone ambao ni moja kati ya mikondo maarufu duniani.
Mwendeshaji wa Yamaha Fabio Quartararo alishinda mbio za mwaka jana za British MotoGP. Alex Rins wa Suzuki na Aprilia wa Aleix Espargaró walimaliza katika nafasi ya pili na tatu mtawalia.
Mbio za hivi karibuni za msimu wa 2022 kufanyika zilikuwa Dutch MotoGP, zikijulikana kama Motul TT Assen vile vile na ziliandaliwa mwezi Juni 26.
Hakimiliki ya picha: Getty Images
Francesco Bagnaia wa Ducati aliibuka na ushindi wa mbio za Dutch MotoGP 2022, ikiwa ni ushindi wa tatu wa msimu kwa raia huyo wa Italia baada ya kushinda mbio za Italian MotoGP pamoja na Spanish MotoGP.
Marco Bezzecchi wa Ducati alimaliza katika nafasi ya pili kwenye mbio za Dutch MotoGP huku Maverick Viñales wa Aprilia akichukua nafasi ya tatu katika mbio hizo za kuvutia.
Mwendeshaji wa Yamaha Fabio Quartararo ambaye pia alishinda mashindano ya dunia ya MotoGP ya mwaka 2021 anasalia kileleni mwa jedwali la waendeshaji akiwa na alama 172.
Aleix Espargaro wa Aprilia, waendeshaji wawili wa Ducati Johann Zarco na Bagnaia wanashika nafasi ya pili, tatu na nne kwa alama 151, 114 na 106 mtawalia.
“Ilitisha sana. Nilitazama kiwambo mara moja na kumuona Alex nje ya mkondo na pikipiki ya samawati,” Bagnaia alisema huku akizungumzia mbio za Dutch MotoGP.
“Niliwaza kuwa alikuwa Fabio na Alex. Tulikuwa na bahati kidogo kusema kweli. Nilitakuwa kutulia na kuzingatia mbio zangu lakini Marco Bezzecchi alikuwa na kasi sana kupunguza nafasi iliyokuwa kati yetu.
“Nilifanya juhudi nyingi ili kupanua nafasi hiyo zaidi kwa maarifa ili kuwa na utulivu sehemu za mwisho za mbio hizo. Mvua ilianza kunyesha na nikalazimika kupunguza kasi. Bezzecchi alikuwa akijitahidi sana kunifikia tena,” aliongeza.
“Haikuwa rahisi. Nilihofia kupata ajali tena. Jambo la msingi sasa lilikuwa kumaliza mbio. Haikuwa rahisi lakini nilijitahidi kumudu kasi pasi na kupita kiwango.”
Ducati wanaongoza kwenye jedwali la kampuni wakifuatiwa katika nafasi ya pili na Yamaha huku nafasi ya tatu ikitwaliwa na Aprilia.
Matokeo ya mbio za British MotoGP 2021
Mshindi: Fabio Quartararo - Yamaha
Nafasi ya pili: Aleix Espargaro - Aprilia
Nafasi ya tatu: Johann Zarco - Ducati
Bashiri Motosport na Betway
Betway inakupa uwezo kubashiri mechi zaidi ya 1,000 kwenye michezo zaidi ya 100. Iwe ni soka, motorsport, mpira wa kikapu, rugby au mchezo wowote unaoupenda, utapata machaguo bora yenye odds bora zaidi.
Kwa habari zote za michezo, taarifa za kubashiri na promosheni tufuatilie Betway kwenye kurasa zetu za Facebook, Twitter, Instagram na Youtube. Pakua App ya Betway.